Home | Terms & Conditions | Help

November 21, 2024, 4:38 pm

NEWS: MBUNGE ATAKA UCHUNGUZI KABLA YA TANESCO KULIPA MABILIONI YA PESA

Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpinga, ameishauri Serekali kufanya uchunguzi kwanza kabla ya kuanza kufanya malipo ya TZS 356b Baada ya Ripoti ya CAG 2020/21 kubaini Serikali imemriwa kuilipa kampuni ya Symbion Power Sh. 356 bilioni, baada ya kuvunja mkataba wake na shirika la Umeme Tanzania (TANESCO)

“uchunguzi ufanyike tujue kilichojificha nyuma.”

Aidha Mpina amesema kuwa kuna wizi na ufisadi mkubwa unafanyika wakati wa uingizwaji wa mafuta nchini kitendo ambacho Waziri mwenyedhamana (Januari Makamba) amekaa kimya.

"Kuna wizi mkubwa unaofanywa kwenye uagizwaji mafuta,lakini hakuna ukaguzi unafanyika na hoja hiyo imezimwa,lakini hatuzungumzii wizi huu,badala yake tumehamishia mjadala kwenye kupunguza tozo kwenye mafuta" Luhaga Mpina

"Waziri anawajua waagizaji wa mafuta nje ya nchi, na anasema wamepandisha bei,je Waziri anataka kusema hawa watu wanaizidi nguvu serikali? Ama ana ubia nao? kwanini waziri anawaogopa hawa na kuwaacha watu wachache waliokaa na kuamua wapandishe bei?" Mhe.Mpina