- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MBUNGE ATAKA KUANZISHWA KWA MAHAKAMA YA FAMILIA
Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) Kupitia Asasi za Kiraia Tanzania Bara (NGOs) Neema Lugangira ameitaka Serikali kuanzisha Mahakama ya Familia (Family Court) kama ilivyofanya kwenye Mahakama za Ardhi ili kusaidia kuondoa changamoto zinazojitokeza ikiwemo Masuala ya Matunzo ya Watoto katika Familia kati ya baba na mama.
Amesema ili Matunzo ya Watoto yaweze kubebwa kwa uzito unaostahili na kupanua wigo mpana wa haki ili kuhakikisha changamoto za namna hiyo zinaondoka kwenye jamii badala ya kuendelea kuwepo kila wakati.
Mbunge huyo aliyasema hayo leo hii May 21, 2021 Bungeni Jijini Dodoma wakati alipouliza Maswali Mawili ya Nyongeza baada ya Serikali kuwasilisha Majibu ua Swali lake la Msingi lililouliza "Je, Serikali ina mkakati gani wa kuwakomboa Wanawake wanaobebeshwa mzigo mkubwa wa kugharamia matunzo ya Watoto bila msaada wa Baba?"
Mbunge Neema alisema pamoja na majibu mazuri ya Serikali lakini hata kwa Sheria zilizopo bado kuna changamoto kubwa kwenye eneo hilo.
Mbunge Neema Lugangira alisema ndio maana hata Chama cha Mapinduzi (CCM) kwenye Ilani yake ya Uchaguzi 2020/2025 imeliona hilo na imeahidi kuielekeza Serikali kwenye Ukarasa wake wa 145 unaosema "CCM itaelekeza Serikali kuimarisha huduma za usuluhuhi wa migogoro ya ndoa na matunzo kwa watoto" na kwa msingi huo aliuliza maswali yake mawili ya nyongeza.
Katika maswali yake ya nyongeza Mbunge Lugangira aliishauri Serikali iboreshe Sheria zilizopo ili gharama za matunzo ya watoto iendani na hali ya uchumi wa sasa na maisha ya sasa kutokana na maisha kuwa juu kuliko ilivyokuwa awali.
Akijibu Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Wazee na Watoto, Mhe Mwanaidi Khamisi amesema "Serikali imetoa maelekezo wazazi kuhakikisha mtoto anapata matunzo yote stahiki, na kama wazazi wa mtoto hawaishi pamoja na mtoto anaishi na Mama yake basi Baba atawajibika kugharamia malezi ya mtoto kulingana na kipato alichonacho". Swali hili pia lilimnyanyua Mhe Waziri Dkt Dorothy Gwajima ambae alisema "Nakiri tatizo Watoto kutelekezwa ni kubwa na ipo haja ya Serikali kufanya harakati za ziada