Home | Terms & Conditions | Help

November 22, 2024, 8:21 am

NEWS: MBUNGE AITAKA SEREKALI KUELEZA UGONJWA UNAOUWA KWA CHANGAMOTO ZA KUPUMUA

Dodoma.Mbunge wa Mbulu Mjini (CCM), Zacharia Isaay ameitaka Serikali ya Tanzania kueleza kinagaubaga kuhusu ugonjwa uliopo sasa hivi nchini uliopewa jina jipya la changamoto za kupumua ambao anasema unaomaliza watu wangi wa jimboni kwake.

"Serekali iache kigugumizi jimboni kwangu watu wanakwisha Spika,nimechoka kuzika hata leo wanazika mtoto wa diwani wakati mwingine nashindwa kukuaga Spika kwenda Mbulu naamua kutoroka,"amesema Isaay.

Isaay ametoa kauli hiyo bungeni hii leo Alhamisi Februari 11,2021 akisema hawezi kulifumbia macho swala hilo kama watamchukia wamchukia lakini ameshasema huku akiongezea kusema kuwa hawezi kuzungumzia mpango mbadala anaona bora azungumzie hali ya wananchi wake ambao kila mara anakwenda kuzika.

Mbunge huyo anasema wanaopoteza maisha jimboni kwake magonjwa yao yanafanana ambayo ni tatizo la kupumua akihofia kuwa msimu wa baridi jimboni kwake utaendelea kuwaumiza.

"Jana nilikwenda hospitali ya hapa Benjamin Mkapa (Dodoma) kwa ajili ya kufanya vipimo lakini wakaniambia mitungi ya gesi imejaa,watu ni wengi sasa nimesema kama watu watanichukia basi lakini nimesema," amesema Isaay.