Home | Terms & Conditions | Help

November 23, 2024, 12:59 pm

NEWS: MBUNGE AIBUA UFISADI WA BILIONI 300 ZA HALMASHAURI

Dodoma. Mbunge wa Makete Festo Sanga ameibua ufisadi mkubwa wa Tsh Bilioni 300 ambazo ni fedha za Umma zilizotengwa kwa ajili ya Vijana,wanawake na Walemavu zinazokwenda katika halimashauri zote nchini maarufu kama asilimia 10.


Akichangia Wizara ya TAMISEMI hii leo Aprili 14, Sanga amesema tangu Mwaka 2017/2018 Serikali kupitia Halmashauri nchini imekopesha zaidi ya Bilioni 300 kwa Makundi ya Vijana, wanawake na watu wenye Ulemavu.

Katika fedha hizo Serikali imefanikiwa kurejesha kiasi cha Billion 96 tu, fedha zingine zote zimezama kwenye mifuko ya watu wahuni.