Home | Terms & Conditions | Help

April 4, 2025, 7:36 am

NEWS: MBUNGE AFARIKI KABLA YA VIKAO VYA BUNGE

Spika wa Bunge la Tanzania Job Ndugai ametangaza kifo cha Aliyekuwa Mbunge wa viti maalum, (CCM), Martha Umbulla, aliyefariki dunia nchini India alipokuwa akipatiwa matibabu.

Kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa na Bunge la Tanzania marehemu ameaaga duni usiku wa kuamkia leo Januari 21, 2021 katika hospitali ya HCG Mumbai.

Spika wa Bunge Job Ndugai ameeleza kupokea kwa mshutuko taarifa hizo na kutoa pole kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki, wabunge pamoja na wananchi wa mkoa wa Manyara kwa msiba huo mzito.

Aidha Ofisi ya bunge ikishirikiana na familia itaratibu mipango ya mazishi na kuendelea kutoa taarifa zitakazo kuwa zikijiri.