- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MBUNGE ACHOMWA KISU BUNGENI
Mbunge wa Uingereza kutoka chama cha Conservative David Amess, 69, amefariki dunia mara baada ya kuchomwa kisu wakati akiwa katika shuguli za Bunge katika eneo alikochaguliwa huko Leigh-on-Sea, mashariki mwa London jana Ijumaa Oktoba 15, polisi ya Uingereza imetangaza.
Kulingana na ushahidi wa kwanza, tukio hilo lilitokea saa sita mchana: Mbunge David Amess alipigwa kisu mara kadhaa wakati alikuwa katika shughuli za bunge. Mbunge huyo mwenye umri wa miaka 69 alikuwa amewapokea watu wake waliompigia kura katika kanisa la Methodist huko Leigh-on-Sea, Essex, mashariki mwa London.
"Alifanyiwa matibabu katika wodi ya wagonjwa mahututi, lakini kwa bahati mbaya, alifariki papo hapo," polisi imesema kuhusu mbunge huyo. “Kijana wa miaka 25 amekamatwa haraka kwa tuhuma za mauaji baada ya polisi kufika katika eneo la tukio. Na kisu kimepatikana. "
Uchunguzi "unaongozwa na maafisa kutoka idara ya kukabiliana na ugaidi" na "itakuwa kazi ya wachunguzi kubaini ikiwa kitendo hiki ni cha kigaidi au la," mkuu wa polisi wa eneo hilo Ben Julian Harrington amesema katika mkutano na waandishi wa habari Ijumaa jioni.