Home | Terms & Conditions | Help

November 23, 2024, 10:02 pm

NEWS: MBOWE AVAMIWA NA KUSHAMBULIWA NA WATU WASIOJULIKANA

Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema na Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe amevamiwa na kujeruhiwa vibaya na watu wasiojulikana usiku wa kuamkia leo Dodoma.

Taarifa rasmi za awali kutoka katika chama chake Chadema na kwa watu wa karibu wa Mbowe zinaeleza kwamba tukio hilo lilitokea wakati kiongozi huyo akirejea nyumbani kwake wakati akitoka kwenye majukumu yake ya kikazi.

Kwa mujibu wa taarifa hizo Mbowe amelazwa katika hospitali ya Ntyuka iliopo pembeni kidogo na jiji la Dodoma akiendelea na matibabu huku mguu wake mmoja ukiwa umevunjika.

Taarifa ya Kamanda wa Polisi Mkoani Dodoma Giles Muroto amesema kuwa wamepata taarifa ya kuwa kiongozi wa kambi rasmi Bungeni Freeman mbowe amevamiwa na wamemkuta ameumizwa na kuvunjwa mguu wa kulia

"Zipo taarifa kwamba Mhe.Mbowe amevamiwa na watu watatu wakamkanyaga kanyaga na kumvunja mguu wa kulia" amesema Muroto

Kamanda Muroto ameswma wanaendelea na uchunguzi juu ya swala hilo la kushangaza "lakini tunafuatilia tutatoa taarifa baadae..hali yake ni nzuri tu". amesema Kamanda wa Polisi Dodoma-Giles Muroto