Home | Terms & Conditions | Help

November 22, 2024, 8:15 pm

NEWS: MBOWE ASHTAKIWA KWA KESI YA UGAIDI

Jeshi la Polisi limesema kuwa linamshikilia Mwenyekiti wa Chadema Taifa Freeman Mbowe kwa tuhuma za kupanga njama za kufanya vitendo vya kigaidi ikiwemo kuua viongozi wa Serikali.

Jeshi limesema kuwa Kiongozi huyo wa Upinzani alikuwa akichunguzwa kwa muda mrefu na kukamatwa kwake huko mkoani Mwanza hakuna mahusiona na kongamano la Katiba Mpya.

Mbowe alikamatwa Juzi na Polisi akiwa jijini Mwanza saa chache kabla ya kuhudhuria mjadala wa kongamano la Katiba Mpya na akasafirishwa kwenda Dar es saalam kwa kuwa kulikuwa na mahojiano ya kufanyika Dar es salaam ambapo ndio nyumbani kwake.

Kwa upande wa chama chake Cha Chadema kimedai katika ripoti yake kwamba, nyumba ya Mbowe ilikaguliwa kwa muda wa saa mbili na Polisi walichukua vifaa kadhaa ikiwemo laptop na tablets zake ambazo huwa anatumia.