Home | Terms & Conditions | Help

November 22, 2024, 2:21 am

NEWS: MBOWE ASHINDA PINGAMIZI LEO JAN 10, 2022

Dar es salaam. Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi leo Jumatatu Januari 10, 2022 imekubali pingamizi la kutopokea sare za Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kama moja ya kielelezo lililowekwa na upande wa utetezi katika kesi inayomkabili Mwenyekiti wa Chama kikuu cha Upinzani Chadema, Freeman Mbowe na wenzake watatu.

Uamuzi huo umetolewa na leo Jumatatu Januari 10, 2022 na Jaji Joachim Tiganga anayesikiliza kesi hiyo.

Katika pingamizi hilo upande wa utetezi uliiomba Mahakama isipokee kielelezo hicho kwa kuwa hakikufuata utaratibu wa ukamataji wa mali wakati upande wa mashtaka ukiiomba mahakama hiyo izipokee sare hizo zinazodaiwa kukutwa na mshtakiwa wa kwanza katika kesi hiyo ya Uhujumu Uchumi, Halfani Bwire Hassan, ziwe kielelezo cha ushahidi wake.

Uamuzi wa Jaji Tiganga "Katika hali ya kawaida Mahakama ilitakiwa kuishia hapa, lakini kuna mwaliko wa Kibatala kuwa Mahakama izingatie kuwa unatafuta nini kila inapokuwa Sheria inakiukwa lakini wanapewa nafasi upande wa mashtaka"