- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MBOWE ALISHUKURU JESHI LA POLISI KWA KUMLINDA
Mwenyekiti wa Chama kikuu cha upinzani nchini Chadema taifa Freeman MBowe amelishukuru Jeshi la Polisi mkoani Mtwara kwa kuhakikisha yeye na msafara wake wanakuwa salama hata kwenye vikao vyao, tangu alipoingia Wilayani Masasi.
Mbowe amesema kuwa wamekuwa na urafiki na Polisi tofauti na siku za nyuma ambapo kuwa na uhasama kati ya Polisi na wananchi au vyama vya Upinzani.
"Mimi na msafara wangu tutakuwa hatutendi haki kama hatutoa shukrani za kipekee kabisa kwa wenzetu wa Polisi wametupa ushirikiano sana hapa Masasi, wamehakikisha usalama wetu wa msafara na usalama wa vikao vyetu." Freeman Mbowe.
Kauli hiyo ya Mbowe ameitoa leo hii Juni 16, 2021 akiwa ziarani Kanda ya Kusini(Mtwara, na Lindi) katika Kampeni ya tunasonga kidijitali.
"Zamani ulikuwa ukiona gari la Polisi limepaki njee, watu wamekaa ndani wamenuna, wamevaa miwani, wamevaa mabomu unauliza Jamani tupo kosovo, na hali hiyo ilikuwa nchi nzima, lakini tumekuja hapa Maaskari wanafuraha na Sisi tunafuraha" amesema Mbowe.