Home | Terms & Conditions | Help

April 5, 2025, 2:04 am

NEWS: MBOWE AACHILIWA HURU

Dar es salaam. Mahakama kuu ya Tanzania Divisheni ya Rushwa na Uhujumu Uchumi imemuachilia huru Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe na wenzake watatu mara baada ya Mkurugenzi wa Mashitaka Nchini DPP, kumfutia mashtaka yote ya Ugaidi na Uhujumu Uchumi yaliyokuwa yakimkabili kwa kuwa hana nia ya kuendelea na kesi hiyo.

Hata hivyo Washtakiwa hao hawakufikishwa Mahakamani leo kwa sababu Mshtakiwa wa 4 Freeman Mbowe ni mgonjwa kwa mujibu wa taarifa ya Afisa Magereza.

DPP ameondoa mashtaka hayo mbele ya Jaji Joachim Tiganga ambaye anasikiliza kesi hiyo namba 16 ya mwaka 2021 ambapo Washtakiwa hao leo walipaswa kuanza kujitetea.