- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MBINU MPYA KUZUIA ONGEZEKO LA WATOTO WA MITAANI.
DODOMA; Serikali kwa kushirikiana na Wadau wa kutokomeza watoto wanaoishi mitaani wameazimia kuanza ukaguzi wa magari ya abiria ili kubaini usafirishaji wa watoto kwa lengo la kuzuia ongezeko la watoto wanaoishi na kufanya kazi mitaani.
Hayo yamefikiwa katika kikao cha pamoja cha Makatibu Tawala wa Mikoa, Makamanda wa Polisi na Wadau wanaoshughulika na kutokomeza watoto wanaoishi mitaani, kilichofanyika Jijini Dodoma.
Katika kikao hicho, wamekubaliana kuwa Jeshi la Polisi lianze kutambua watoto wote wanaoishi na kufanya kazi mitaani ili kuwarejesha kwenye familia zao na kuiomba Wakala wa usafirishaji LATRA na Wadau wa usafiri kuweka mfumo madhubuti wa usafirishaji watoto.
Wamesema ukaguzi wa vyombo vya usafiri hautahusisha ubovu tu wa magari bali hadi kwenye Chesesi ili kubaini usafirishaji wa watoto,ikiwezekana kuwekwa utaratibu wa kuandika umri wa wasafiri.
Aidha, Wadau hao wamesisitiza Jamii kuhamasishwa zaidi kuhusu malezi, matunzo na ulinzi ya watoto kupitia mbinu mbalimbali ikiwemo vyombo vya Habari na nyumba za Ibada.
Kwa upande wake Kamishna wa Utawala na Rasilimali watu Kamanda Benedict Wakulyamba ameishukuru Wizara kwa kuwashirikisha wakiwa ni Wadau muhimu katika kumaliza changamoto hiyo kwani Jeshi la Polisi linahusika moja kwa moja na makundi yanayoshughulikiwa na Wizara na jukumu lao ni kuhakikisha wanatoa ushirikiano wa kutosha kutokomeza tatizo hili.
Akihitimisha kikao hicho Katibu Mkuu Dkt. Jingu, amesema kuna kila sababu ya kuwalea watoto vizuri ili kuondokana na changamoto hiyo na kuwahamasisha Wadau wote kuweka nia thabiti ya kupambana na tatizo hilo kikamilifu.
"Tumefikia Maazimio ya jumla ya kila Taasisi na kama yatatekelezwa ipasavyo uwezekano wa kuondokana na changamoto hii ya Watoto waishio katika Mazingira hatarishi ni mkubwa” alisisitiza Dkt Jingu.
Akiwasilisha mada kuhusu haki ya mtoto, Mkurugenzi wa Kitengo cha Sheria kutoka Wizara ya Afya- Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Lucy Saleko alisema Sheria ya Mtoto ya Mwaka 2009 inawataka wazazi kuwajibika kuwalinda watoto wao dhidi ya ukatili na unyanyasaji wa aina yoyote vinginevyo watachukuliwa hatua.