Home | Terms & Conditions | Help

November 27, 2024, 6:11 am

NEWS: MBATIA AFUNGIWA SIKU 7 KUFANYA KAMPENI

Vunjo. Mgombea ubunge wa jimbo la Vunjo wilaya ya moshi Mkoani Kilimanjaro kwa tiketi ya NCCR-Mageuzi, James Mbatia amesimamishwa kufanya kampeni kwa siku saba, kuanzia leo hii Oktoba 17 hadi 23, 2020.

Mbatia anakuwa ni Mgombea wa tatu kufungiwa kufanya kampeni kwa Tanzania Bara na Niwanne kwa Jamhuri ya muungano wa Tanzania.

Mbatia ambaye pia ni mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi amethibitisha kusimamishwa kuendelea na kampeni leo Oktoba 17,2020 baada ya kukabidhiwa barua.

“Ni kweli wamenisimamisha lakini nimeshangaa maana walipotaka nipeleke utetezi kuhusu hicho kipeperushi tuliwapelekea na ushahidi wa barua iliyokitambulisha hicho kipeperushi,” amesema Mbatia.

Barua ya mwenyekiti wa kamati ya maadili jimbo la Vunjo, Michael Mwandezi inaeleza kuwa Mbatia amesimamishwa kufanya kampeni kutokana na kutumia kipeperushi ambacho hakijaidhinishwa na msimamizi wa uchaguzi.

Kwa mujibu wa mwenyekiti huyo, kamati ya maadili katika kikao chake cha Oktoba 16, 2020 ilikaa na kupitia tuhuma za uvunjifu wa maadili ya uchaguzi na kumkuta na hatia ya kukiuka maadili hayo.