- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
News: Mawazo ya Wahasibu Yasikilizwe Kabla Maamuzi ya Kiutendaji Hayajafanyika - Dkt. Biteko
DODOMA: Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko ametoa rai kwa viongozi mbalimbali nchini kusikiliza mawazo ya Wahasibu kabla hawajafanya maamuzi yoyote ya kiutendaji kwani hiyo ni moja ya jukumu linalokana na taaluma yao.
Ametoa rai hiyo jana Desemba 04, 2024 jijini Arusha wakati akifunga Mkutano wa Pili wa Mwaka wa Jumuiya ya Wahasibu Wakuu wa Afrika (AAAG) uliofanyika kuanzia Desemba 02 hadi 05, 2024.
Dkt. Biteko amesema kuwa, mahali popote pa kazi ili kuwe na ufanisi, ni lazima Wahasibu watambulike na waheshimiwe ili watoe matokeo yanayokusudiwa kwani kama hakuna taaluma ya Uhasibu, rasilimali haziwezi kusimamiwa vizuri na matokeo yake kutakuwa na lawama zisizokuwa na sababu.
"Kazi ya Wahasibu ni kushauri, unawashauri wakuu wako kiuchumi ili wafanye maamuzi yaliyo sahihi. Kuna wakati Mhasibu ndiyo anashauriwa ili kufanya maamuzi, hii siyo sahihi na tukibadili mfumo, tutapata matatizo", amesema Mhe. Biteko
Amesisitiza kuwa, taaluma hiyo ni muhimu hivyo waisimamie bila uoga, watumie fedha za taasisi kwa malengo yaliyokusudiwa na wajitahidi kuzuia hasara pamoja na kufuata utaratibu uliowekwa.
Vile vile, ameeleza kuwa Mhasibu asiyejiendeleza ili kuendana na teknolojia na mabadiliko ataachwa nyuma, hivyo ni lazima kuendelea kujifunza kwa njia mbalimbali ambapo kuhudhuria mikutano kama hii ni muhimu ili muendelee kuboresha maarifa yenu.
Kwa upande wake Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Hamad Chande amesema uwepo wa Wahasibu Wakuu wa Serikali Afrika na taaluma zao katika mkutano huo, utawanufaisha wananchi wengi na watarejesha imani zao kwa serikali na kwa Wahasibu wote.
Nawaomba Wahasibu Wakuu wa Serikali mlioshiriki mkutano huu kufikisha ujumbe kwa Wahasibu wasaidizi wa sekta mbalimbali kuwa Mungu anawaona kwa kila wanachokifanya, hivyo wafanye yale ya halali." Amemalizia Mhe. Chande.
Naye Mhasibu Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, CPA. Leornad Mkude amesema Mkutano huo umekuwa na mijadala mbalimbali iliyohusiana na fursa na changamoto za uhasibu zilizopo katika maeneo yao ya kazi ili kupata suluhu na kufikia kwa pamoja ndoto ya Umoja wa Afrika kupitia Wahasibu Wakuu.
Amewasihi washiriki kuchukua ujuzi na mawazo waliyoyapata na kuyapeleka katika nchi zao ili kazi ya Uhasibu iendelee kufanyika kwa ufanisi mkubwa.