- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MATUMIZI YA KINGEREZA MAHAKAMANI YAENDELEA KUZUA MJADALA KWA WADAU.
ARUSHA: Kutokana na Mfumo wa utoaji haki nchini kuathiriwa na wakoloni ikiwa ni pamoja na kutumia lugha ya Kingereza Mahakamani hali hiyo imepelekea Wananchi kushindwa kuelewa na kufuatilia mienendo ya mashauri yao.
Akitoa taarifa ya matumizi ya lugha ya kiswahili katika uandishi wa sheria na mfumo wa utoaji haki, Wakati wa Mkutano wa wadau kuhusu masuala ya msaada wa kisheria na upatikani haki kwa wananchi uliofanyika leo Jijini Arusha Wakili wa Serikali Esther Msambazi amesema matumizi ya kingereza katika mahakama zetu umeleta mjadala katika jamii kuhusu mchango wa lugha ya Kiswahili katika kuwasaidia wananchi wa kawaida ,na kutaka kiswahili kitumike ili wananchi waweze kufuatilia mashauri yao mahakamani kwa kuwa ni lugha inayoeleweka na wengi.Msambazi ameendelea kusema hali hiyo imeleta sintofahamu katika jamii na wakati mwingine husababisha kushindwa kufikia haki,na kubainisha kuwa, kutokana nakuwepo kwa azma ya Serikali ya kuendelea kuenzi lugha ya Kiswahili,mwaka 1999 ilitungwa sera ya utamaduni, ambapo sera hiyo iliweka matamko juu ya matumizi ya lugha ya Kiswahili katika Nyanja zote ambayo kama yangefanyiwa kazi hali ya matumizi duni ya Kiswahili iliyopo sasa ingelikuwa ni historia.
''Matumizi ya lugha ya kigeni kwenye mfumo wa utoaji haki umechangia kwa kiasi kikubwa kuwakosesha wananchi haki na fursa ya uelewa wa sheria zinazowaongoza na kushindwa kuelewa na kufuatilia mienendo ya mashauri, Muelekeo huu wa serikali ni muhimu kuzingatia hatua ambayo matumizi ya lugha ya Kiswahili yamefikia na kuwa lugha ya Taifa la Tanzania inayotumika katika Mihimili ya Serikali’’ amesema Msambazi.
Akizungumzia Matumizi ya Kiswahili Mahakamani, Mkurugenzi Mtendaji wa TLS Kaleb Lameck Gamaya, amesema moja ya misingi ya kufikia haki katika mfumo wa utoaji haki ni lugha inayoeleweka kwa mwombaji au mtafuta haki.