Home | Terms & Conditions | Help

November 23, 2024, 7:18 pm

NEWS: MAREKENI YASIKITISHWA NA KUKAMATWA VIONGOZI WA UPINZANI TANZANIA

Taifa la Marekani kupitia Ubalozi wake hapa nchini umesema kuwa umesikitishwa na hatua za hivi karibuni za Serikali ya Tanzania kuminya kwa demokrasia, ikiwa ni pamoja na kuwakamata viongozi wa vyama vya siasa vya upinzani wakiwa katika vikao vyao vya ndani na kufuta leseni ya gazeti la chama cha siasa cha upinzani la Tanzania Daima.

Katika taarifa yake ya Ubalozi iliyotolewa leo asubuhi Juni 25, 2020 imesema kuwa Hatua hizi ni mwendelezo wa mlolongo wa matukio ya kusikitisha ya vitisho kwa wanachama wa vyama vya upinzani, asasi za kiraia na vyombo vya habari.

"Haki ya kukusanyika kwa amani na uhuru wa kujieleza ni mambo yaliyojumuishwa na yanayolindwa na Katiba ya Tanzania na Tamko la Kimataifa la Haki za Binadamu."

"Ubalozi wa Marekani unafahari kusaidia na kuunga mkono uhuru wa kujieleza na ushiriki jumuishi wa kisiasa kwa namna zote"

Tamko hilo la Marekani limejira mara baada ya kuwepo kwa matukio mawili makubwa moja ni Kitendo cha Jeshi la Polisi Nchini Juzi Juni 23, kumkamata Kiongozi Mkuu wa chama cha ACT Wazalendo na wanachama wengine 7 kwa madai ya Kufanya maandamano Bila Kibali, hatua ambayo vyama vingi vya upinzania na wanaharakati ndani na Njee ya nchi walilaani vikali na kutaka kuwepo mazingira ya haki kwa viongozi hao.

Tukio la pili ni Saa chache Mara tu baada ya kutokea Tukio hilo la ACT, Serekali hapa nchini ilitangaza kulifungia gazeti la kila Siku la Tanzania Daima kwa kile kilichodaiwa kuwa Gazeti hilo limekuwa na mwenendo wa kuandika habari zinazokinzana na Sheria ya Habari ya mwaka 2016, huku Serekali ikitanabaisha kwamba Gazeti hilo licha ya kupewa onyo mara kadhaa lakini Uongozi wa Tanzania Daima umekuwa ukikaidi na kudharau mamlaka za nchi.

Siku inayofuata mara baada ya Serekali kulifungua Gazeti hilo Chama kikuu cha Upinzania nchini cha Chadema kilitoa taarifa yake Juu ya uwamuzi huo wa Serekali na kulaani vikali hatua hiyo ya Serekali ya Kulifungia Gazeti hilo.

Chadema iliitaka Serekali kuzitaja ni habari gani zilizokuwa na shida kufanya gazeti hilo kulifungia sambamba na hilo ikaitaka Serekali pia kutaja makosa yaliyofanywa na Tanzania Daima.