- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MAREKANI YAWAONYA RAIA WAKE DHIDI YA KUSAFIRI KENYA
Wizara ya mambo ya nje ya Marekani imewaonya Raia wake kutosafiri nchini Kenya kwa wakati huu, kutokana na kushamiri kwa majanga ya Covid-19, uhalifu, ugaidi na utekaji nyara.
Taarifa ya tahadhari ambayo imetolewa na wizara hiyo inawashauri wamarekani kutojielekeza kwenye eneo la mpaka kati ya Kenya na Somalia na kwenye maeneo ya pwani kutokana na ugaidi.
Wizara hiyo imewasihi raia wa Marekani kuchukua tahadhari kubwa wanaposafiri nyakati za usiku kila mahali nchini humo kwa sababu za uhalifu, pia wajiepushe kwenda mitaa ya Eastleigh na Kibera, mjini Nairobi kutokana na vitendo vya uhalifu na utekaji nyara.
Uhalifu mbaya kama vile wizi wa magari kwa kutumia silaha, uvamizi wa majumbani na utekaji nyara, unaweza kutokea wakati wowote, taarifa hiyo ya wizara ya mambo ya nje imesema