- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MAREKANI YAMUUA KIONGOZI WA AL QAIDA
Rais wa Marekani Joe Biden usiku wa kuamkia leo Agosti 2,2022 ametangaza kuuwawa kwa kiongozi wa kundi la al-Qaida, Ayman al-Zawahiri na mashambulizi ya ndege yasiyo na rubani ya Marekani mjini Kabul, nchini Afghanistan, huku Saudi Arabia ikisifia kifo hicho.
Akizungumzia kutokea Ikulu ya White House usiku wa kuamkia Jumanne (2 Agosti), Biden aliitaja operesheni iliyomuua Zawahiri mjini Kabul kwamba imetenda haki na italeta faraja kwa familia za wahanga wa mashambulizi ya Septemba 11 mwaka 2001 nchini Marekani.
Mbali ya mashambulizi hayo ya Septemba 11, Biden ametumia sababu nyengine ya ziada kuhalalisha uamuzi wake wa kuamuru mauaji ya Zawahiri. "Alifanya video, zikiwemo za wiki za hivi karibuni, akiwataka wafuasi wake kuishambulia Marekani na washirika wetu. Sasa, haki imetendeka na kiongozi huyu wa kigaidi hayupo tena." Alisema.
Akielezea undani wa mashambulizi hayo ya ndege zisizo rubani yalivyofanyika, Biden alisema maafisa wa ujasusi wa nchi yake waliifuatilia nyumba ya Zawahiri katika mtaa mmoja wa Kabul, ambako alikuwa akijificha na familia yake, na baadaye yeye Biden akaidhinisha operesheni hiyo wiki iliyopita na ikatekelezwa juzi Jumapili.
"Operesheni hii ilipangwa kwa uangalifu, na kwa kiwango kikubwa imepunguza madhara kwa raia wengine. Na wiki moja iliyopita, baada ya kushauriwa kwamba mazingira yalikuwa sahihi, nilitowa idhini ya mwisho ya kumpata, na operesheni imefanikiwa. Hakuna hata mtu mmoja wa familia yake aliyeumizwa na hakuna madhara yoyote kwa raia." Alisema Biden.