Home | Terms & Conditions | Help

November 21, 2024, 4:53 pm

NEWS: MAREKANI NA UINGEREZA ZASHIKIANA KUZUIA KOMBORA LA HYPERSONIC LA URUSI

Uingereza, Marekani na Australia zimepanga kuungana kushirikiana kufanya utafiti wa namna ya kuzuia silaha za hypersonic zinazomilikiwa na Urusi ili ziweze kujilinda dhidi ya silaha hizo.

Mpango huo utakuwa sehemu ya ushirikiano wa AUKUS, mkataba wa usalama uliotangazwa na nchi hizo tatu mwaka jana.

Hatua hiyo ni nikufuatia hatua za Urusi na China kustawisha kwa kasi makombora ya hypersonic na matumizi yao yaliyodaiwa na Urusi nchini Ukraine mwezi uliopita.

Kama haujui Silaha za hypersonic ndugu ni zile zenye kasi mara tano ya sauti.
siliaha za Hypersonic Ni vigumu zaidi kujilinda dhidi yao kwa sababu ya kuwa na kasi na vilevile yanaruka katika mwinuko wa chini - nje ya mstari wa kuonekana kwa rada za ardhini - na yanaweza kurushwa katikati ya ndege.

Uingereza kwa sasa haina makombora ya hypersonic.

Marekani na Australia zina mpango wa pamoja wa kutengeneza silaha lakini serikali ya Uingereza ilisisitiza lengo la mradi huo mpya litakuwa katika ulinzi.

Ilisema hakuna mipango ya Uingereza kuunda silaha zake za hypersonic lakini mpango huo mpya utasaidia kutathmini ikiwa itahitaji kuzitengeneza katika siku zijazo.

Imeongeza kuwa tangazo la hivi punde halihusiani na utumiaji wa silaha za Urusi nchini Ukraine lakini ilisema ukweli kwamba mataifa mengine yalikuwa yakiwekeza katika silaha hizo inamaanisha kwamba Uingereza inapaswa kufikiria jinsi ya kujilinda dhidi yao.

Mnamo tarehe 19 Machi, Urusi ilidai kutumia kombora la hypersonic kuharibu ghala la silaha magharibi mwa Ukraine, na ujasusi wa jeshi la Marekani umependekeza kuwa vikosi vya Urusi vimezitumia mara kwa mara tangu wakati huo.

Mashambulizi hayo yaliashiria matumizi ya kwanza ya makombora ya hypersonic katika mapigano.