- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MARAIS WA NCHI ZA SADC WAKUTANA HII LEO
Viongozi wakuu sita wa Afrika wanaounda Jumuiya ya maendeleo kusini mwa Afrika (SADC) watakutana katika mji mkuu wa Msumbiji , Maputo,ambapo kutakuwa na mkutano wa dharura unaoangazia mashambulizo yanayotokea kusini mwa Afrika, tovuti ya serikali ya Zimbabwe imeripoti.
Jumuiya ya maendeleo kusini mwa Afrika (SADC) imeitisha mkutano huo wa Extraordinary Double Troika Rais wa Botswana Mokgweetsi Masisi. Ukiondoa Msumbiji ambaye ndio mwenyeji, mataifa mengine yatakayokuepo katika mkutano huo ni Afrika Kusini, Botswana, Zimbabwe, Malawi na Tanzania.
Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnagngawa tayari ameondoka katika kikao hicho.
Awali rais wa Msumbiji Filipe Nyusi alisema ataitisha mkutano wa baraza la ulinzi na usalama lakini hakuweka wazi ni lini mkutano huo utafanyika.
Wanamgambo wa kiislamu walivamia mji wa Palma uliopo kaskazini mwa jimbo la Cabo Delgado Machi 24, na kuuwa watu kadhaa na mamia kulazimika kukimbia makazi yao huku wengine wakikimbilia Tanzania.
Kundi la wanamgambo wa kiislamu (IS) walidai kuhusika na shambulio hilo.
Kundi hilo la wanamgambo wa kiislamu limlenga eneo hilo tangu Oktoba mwaka 2017, na hivi karibuni shambulio lao lililazimisha kampuni kubwa ya nishati ya Ufaransa kusitisha mipango yake ya uzalishaji wa gesi asilia katika eneo la Afungi Peninsula.