Home | Terms & Conditions | Help

April 4, 2025, 7:31 am

NEWS: MAPACHA WALIOUNGANA IRINGA WAFARIKI DUNIA

Watoto Mapacha wawili walioungana jina Dorcas na Dorine wamefariki dunia hii leo katika hospitali teule ya wilaya ya Iringa Tosamaganga.

Kwamujibu wa Taarifa iliyotolewa na Mganga Mfawidhi wa hospitali hiyo Dokta Ismail Banoba imesema kuwa mapacha hao wamefariki baada ya kupata changamoto ya upumuaji.

Januari 19, 2021 serikali wilayani Iringa iliwakabidhi watoto hao mapacha walioungana, Dorcas na Dorine kwa masista wa shirika la Theresia wa mtoto Yesu ili kuwalea watoto.

Ikumbukwe tu kuwa shirika hilo ndilo liliwalea mapacha wengine Maria na Consolatha ambao waliofariki mwaka 2018 wakiwa na umri wa miaka 21.