- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MAKONDA APEWA SIKU 21 KUWASILISHA HATI KIZANI MAHAKAMANI
Dar ea salaam Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni, Dar es salaam imempa siku 21 aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda, kuwasilisha hati kinzani dhidi ya maombi yaliyofunguliwa na Mwanahabari, mkongwe Saed Kubenea, kutaka kibali cha kumfungulia kesi ya jinai.
Tamko hilo limetoleo hii leo Marchi 2, 2022 mbele ya Hakimu Mkazi, Aron Lyamuya.
Kubenea ambaye amewahi kuwa Mbunge wa Jimbo la Ubungo, anamshutumu Paul Makonda kwa makosa tofauti ikiwemo matumizi mabaya ya madaraka, ukiukwaji wa haki za binadamu pamoja na kuvamia kituo cha Televisheni cha Clouds Media Group na kuingilia urushaji wa matangazo ya kipindi mnamo Machi 17, 2020.
Hapo awali ombi la kufungua kesi hiyo lilikataliwa na mahakama za Hakimu Mkazi Kisutu na Kinondoni kwa madai kuwa ni lazima kuwepo na hati ya mashitaka ya mahakama ya mwanzo.
Pia mahakama hizo zikaendelea kusema hapakua na kiapo cha kuonesha namna gani DPP ameshindwa kuchukua hatua za kumshtaki Makonda.
Katika Shauri la Kubenea, pia anawashitaki Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai DCI na Mkurugenzi wa Mashitaka DPP ambao anadai walishindwa kumchukulia hatua za kisheria Makonda alipotenda makosa hayo.