Home | Terms & Conditions | Help

November 25, 2024, 9:37 am

NEWS: MAKAMBA KUPELEKA GRIDI YA TAIFA KIGOMA MWAKANI

Waziri wa Nishati nchini Januari Makamba ameahidi kupeleka Umeme wa Gridi ya Taifa Mkoani Kigoma ili kumaliza adha na gharama ya Umeme mkoani humo.

Makamba amesema kuwa Tanesco Mkoa wa Kigoma inatumia Tsh bilioni 3 kununua mafuta ya deseli kwa ajili ya kuzalisha umeme kwa wateja 63,000 mkoani humo ambao wanalipa Tsh bilioni 1.5 ambapo kimahesabu ni kwamba Serekali inapata hasara ya Tsh bilioni 1.5 kwa kila mwaka.

Waziri Makamba ametoa kauli hiyo hii leo Octoba 6, 2021 wakatika wa ziara yake Mkoani.

Makamba aliambatana na Mkurungezi mtendaji wa Shirika la Umeme TANESCO Chande, ikiwa ni kufuata maagizo ya Makamu wa Rais Dr. Philip Mpango ya Tarehe 24 Octoba mwaka huu.

"tunamaliza tatizo(Kigoma), Kigoma ipo nje ya Gridi, kwahiyo TANESCO inatumia bilioni 3 kwa mwezi umeme wa dizeli kwa wateja 63,000 wanaolipa bilioni 1.5. Tunaleta Gridi Kigoma

Dk Mpango alisema anataka hadi ikifika Oktoba 15 viongozi hao wampe taarifa kuhusu utekelezaji wa agizo hilo.

Alitoa agizo hilo Kasulu wakati akifungua maonesho ya biashara na viwanda yanayoratibiwa na Shirika la Viwanda Vidogo (SIDO).

Dk Mpango aliagiza hayo baada ya Mbunge wa Kasulu Mjini, Profesa Joyce Ndalichako kumweleza kuwa maagizo aliyotoa kuhusu tatizo la kukatika umeme na kufikisha umeme kwa wananchihalijatekelezwa.

Profesa Ndalichako alisema bado kuna shida ya kupata umeme na wananchi wanahangaika kuungainishiwa nishati hiyo hivyo akaomuomba Dk Mpango atoe maelekezo kuhusu jambo hilo.

"Mheshimiwa Makamu wa Rais binafsi nimetembelea maeneo mbalimbali ya Wilaya Kasulu lakini nimeona mjini Kigoma bado umeme unakatika sana na pia upelekaji wa umeme kwenye maeneo ya wananchi kama ulivyoagiza haujafanyika vya kutosha, naomba upokee taarifa hii na utoe maelekezo yako," alisema.