Home | Terms & Conditions | Help

November 21, 2024, 4:46 pm

NEWS: MAKAMBA ATOA UFAFANUZI KUPANDA BEI YA MAFUTA

Dodoma. Waziri wa Nishati nchini January Makamba, amefafanua kuwa kupanda kwa bei za mafuta nchini inatokana na gharama mbalimbali ikiwemo zile zilizotumika kununulia mafuta, gharama ya usafirishaji na gharama za biashara yenyewe hapa nchini.

Kauli ya Waziri Makamba ameitoa hii leo Mei 5, 2022, bungeni Dodoma, wakati akijibu hoja iliyotolewa na Mbunge wa Kilindi, Omari Mohamed Kigua, ya kusimamisha shughuli za Bunge zilizokuwa zikiendelea ili kujadili hali ya mfumuko wa bei ya mafuta nchini.

"Wote tunajua bei za mafuta zimepanda duniani na sisi kama nchi sio wazalishaji wa mafuta tunanunua mafuta kutoka nje na sehemu kubwa ya bei ya mafuta inayopangwa nchini inatokana na gharama ya mafuta yenyewe, gharama ya kuleta, kodi na tozo mbalimbali na gharama za kufanya biashara yenyewe hapa nchini," amesema Waziri Makamba