- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MAKAMA ZA KIGOMA ZAJIWEKEA KIKIMO CHA KUSIKILIZA KESI
Kigoma. Jaji mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Kigoma Mhe.Jaji Ilvin Mgetta amesema idara ya mahakama mkoani humo imejiwekea malengo ya kumaliza kusikilizwa shauri ndani ya miezi mitatu tangu kufunguliwa kwa shauri katika mahakama ya mwanzo.
Amesema katika mahakama za wilaya, mahakimu wamepewa muda wa miezi mine na mahakama kuu kanda ya kigoma muda wa miezi sita, lengo likiwa kuhakikisha wananchi wanapata haki katika kipindi cha muda mfupi na kwamba hakimu ambaye atashindwa kutekeleza mpango huo hatua za kinidhamu kuhusu utendaji wake zitachukuliwa.
Mgetta ameongea kwa kusema kuwa kufanya hivyo kunawapunguzia Adha na kuleta nafuu kwa wanachi wa mkoa huo.
Amesema haki ya mtu lazima aipate bil kuwepo na usumbufu wa aina yeyote na wao kama Mkoa wa Kigoma wamejipanga kikamilifu kuwa sehemu ya Nafuu kwa wananchi.