- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MAJALIWA AWAONYA VIONGOZI KUTUMIA WALINZI BINAFSI
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameagiza Viongozi wa Serekali kutotumia Walinzi na Waandishi wa Habari binafsi katika Ofisi za Umma kwani ndio watakuwa chanzo cha uvujaji wa siri za Serikali.
Waziri Majaliwa ameyasema hayo kwenye ufunguzi wa mafunzo ya uongozi leo Oct 29, 2021 Dodom.
Majaliwa amesema upo utaratibu wa kufuata endapo itabainika Kiongozi anahitaji kupatiwa Wasaidizi hao hivyo kuwataka Viongozi kuzingatia utaratibu huo na si vinginevyo.
Majaliwa ameyasema leo wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya Mawaziri na Manaibu yanayotolewa Jijini Dodoma “nimedokezwa kuwa lengo la mafunzo haya ni kupanua uelewa wa Mawaziri na Naibu Mawaziri kuhusu masuala mbalimbali yahusuyo uongozi ikiwa ni pamoja na kuelewa majukumu””
“Pia kuelewa madaraka na mipaka ya nafasi zenu, kuongoza Watu, kufanya maamuzi ya kimkakati na kuboresha sifa binafsi za kiuongozi, ni imani yangu kupitia mafunzo haya mtapata ujuzi” amesema Waziri Mkuu Majaliwa.