Home | Terms & Conditions | Help

November 21, 2024, 9:04 pm

NEWS: MAJALIWA AMPA SIKU 7 KATIBU MKUU KUTOA MAELEZO YA KUNUNUA MAGARI KWA GHARAMA KUBWA

Mwanza. WAZIRI MKUU wa Tanzania Kassim Majaliwa ametoa siku saba kuanzia leo Desemba 17 kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu na maofisa wanaochakata maombi ya ununuzi wa magari kueleza kwa sababu gani walinunua magari ya baadhi ya viongozi kwa gharama kubwa sana.

Waziri Majaliwa ametoa agizo hilo hii leo Desemba 17, 2020 wakati akizungumza na watumishi wa umma, wabunge, madiwani katika jiji la Mwanza

Waziri Majaliwa ameyataja Magari yaliyotajwa kununuliwa bei ghali ni ya Ofisi ya Waziri Mkuu na wakurugenzi wa Jiji la Mwanza, Halmashauri ya wilaya ya Chato, Msalala na Kahama.