Home | Terms & Conditions | Help

April 3, 2025, 11:52 am

NEWS: MAHAKAMA YAWARUHUSU KINA MDEE KUUPINGA UWAMUZI WA CHADEMA

Dar es Salaam. Mahakama Kuu kanda ya Dar es salaam imewaruhusu waliokuwa wanachama wa Chadema, Halma Mdee na wenzake 18 kufungua shauri la kupinga uamuzi wa chama hicho kuwavua uanachama.

Mahakama imetoa ruhusa hiyo leo Ijumaa Julai 8, 2022, baada ya kukubaliana na hoja za maombi yao (Mdee na wenzake 18) ya ridhaa ya kufungua shauri hilo la kupinga kuvuliwa uanachama.

Maombi hayo ya kina Mdee yalisikilizwa na Jaji Mustapha Ismail Juni 30 mwaka huu na Chadema kupitia kwa jopo la mawakili wao linaloongozwa na Peter Kibatala, walipinga hoja za mawakili wa kina Mdee kuwa hazikidhi matakwa ya kisheria kupewa ruhusa hiyo

Hata hivyo Jaji Ismail katika uamuzi wake leo amekubaliana na vigezo na hoja zote za kina Mdee, zilizowasilishwa na mawakili wao, Ipilinga Panya, Aliko Mwamanenge, Edson Kilatu na Emmanuel Ukashu.

Kwa uamuzi huo sasa kina Mdee wanatakiwa kufungua shauri lao hilo ndani ya siku 14 kuanzia leo.