- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MAHAKAMA YATUPILIA MBALI PINGAMIZI LA SEREKALI KESI YA KUPIGA MIKUTANO YA KISIASA
Mahakama Kuu kanda ya Dar es salaam, jana imetupilia mbali pingamizi la awali lililowekwa na Jamhuri dhidi ya Shauri la Kikatiba lililofunguliwa na Baraza la Wadhamini la NCCR-Mageuzi linalopinga kitendo cha jeshi la Polisi kuzuia kufanyika kwa mikutano ya vyama vya Siasa nchini.
Kesi hiyo Namba 27 ya 2021 ambayo NCCR Mageuzi imewashitaki Mwanasheria Mkuu wa Serekali, IGP, RPC Kanda Maalum ya Dar es salaam, RPC-Ilala, na OCD-Ilala imeendelea jana Januari 20, 2022 chini ya Jaji JOHN MGETTA ambapo Mahakama imetoa maamuzi ya pingamizi lililowekwa na serikali.
Kesi hiyo imehairishwa na kuoangwa tena mbele ya jopo la majaji watatu tarehe 7 Februari 2022 Saa 8:00 Mchana, katika Mahakama hiyo, kwa ajili ya kupanga tarehe ya kuwasilisha hoja za msingi za namna Jeshi la Polisi lilivyokiuka Katiba na sheria za nchi kwa kuzuia mikutano ya vyama vya siasa nchini.