Home | Terms & Conditions | Help

April 5, 2025, 5:08 pm

NEWS: MAHAKAMA YATUPILIA MBALI PINGAMIZI LA MBOWE

Dar es salaam. Mahakama Kuu ya Tanzania Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi jijini Dar es salaam leo imetupilia mbali pingamizi la upande wa utetezi(Mbowe na wenzake) ya kutaka mahakama hiyo ikatae kupokea kitabu cha kumbukumbu ya mahabusu kutoka Kituo Kikuu cha Polisi kati jijini Dar es Salaam baada ya hoja tatu za upande wa utetezi kukosa mashiko.

Mbowe na wenzake hao, Halfan Bwire Hassan, Adamu Hassan Kasekwa na Mohamed Abdillahi Ling’wenya wanakabiliwa na kesi hiyo inayosikilizwa na Jaji Joachim Tiganga.

Uamuzi huo umetolewa na Jaji Joachim Tiganga wakati akisoma uamuzi wa pingamizi hiyo na kusema kielezo hiko kinapaswa kupolelewa na mahakama kwa kuwa shahidi wa kwanza katika kesi hiyo alitoa kielezo hicho kama utambuzi na sio maombi ya kutaka mahakama kupokea kieleezo hicho cha kitabu cha kumbukumbu ya mahabusu.

Uamuzi huo unahusu pingamizi la mawakili wa utetezi katika kesi hiyo, ambao walipinga kupokewa kwa kitabu cha kumbukumbu za mahabusu (Detantion Register – DR), cha Kituo Kikuu cha Polisi, Dar es Salaam, cha mwaka 2020, kiwe kielelezo cha ushahidi upande wa mashtaka.

Upande wa mashtaka unaongozwa na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Robert Kidando uliiomba mahakama hiyo ikipokee kitabu hicho kuwa kielelezo cha ushahidi wake, kupitia kwa shahidi wa pili katika kesi ndogo ndani ya kesi ya msingi, Ditektivu Koplo Ricardo Msemwa.

Hata hivyo jopo la mawakili wa utetezi linaloongozwa na Peter Kibatala lilipinga kitabu hicho kupokewa, huku wakitoa hoja tatu za pingamizi lao

Walidai kwamba hakuna amri ya mahakama ya kukiondoa mahakamani kielelezo hicho kwa kuwa kilishapokewa mahakamani katika kesi ndogo iliyohusu uhalali wa maelezo ya mshtakiwa wa pili, Adamu Kasekwa.