Home | Terms & Conditions | Help

Sat Apr 05 2025 5:47:48 PM

NEWS: MAHAKAMA YATUPILIA MBALI KESI YA KINA MDEE NA WENZAKE

Dar es Salaam. Mahakama Kuu kanda ya Dar es Salaam hatimaye imeyatupilia mbali maombi ya waliokuwa wanachama wa chama kikuu cha upinzani Chadema wakina Halima Mdee na wenzake kutokana na kasoro katika jina la mjibu maombi wa kwanza.

Viongozi hao wa Baraza la Wanawake wa Chadema (Bawacha) waliomba kibali cha kupinga kufukuzwa uanachama wa Chadema katika mahakama hiyo.

Wajibu maombi walikuwa Bodi ya Wadhamini wa Chadema, Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG).

Chadema kupitia jopo la mawakili wake linaloongozwa na Peter Kibatala waliweka pingamizi wakiiomba Mahakama hiyo isiyasikilize maombi hayo, wakidai kuwa yana kasoro za kisheria huku wakibainisha hoja sita.