Home | Terms & Conditions | Help

November 24, 2024, 9:45 am

NEWS: MAHAKAMA YAMUACHILIA HURU HALIMA MDEE

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Jijini Dar es Salaam, imemwachia huru, Mbunge wa viti maalum Halima Mdee, katika kesi no. 228/2017, inayomkabili ya kumkashifu Rais John Magufuli, baada ya upande wa mashtaka kushindwa kuthibitisha mashtaka yake Mahakamani.

Hukumu hiyo imetolewa hii leo Februari 25, 2021 na hakimu mkazi Mkuu Thomas Simba.

“Upande wa mashtaka umeshindwa kuthibitisha mashtaka dhidi ya mshtakiwa kuwa alitoa maneno machafu dhidi ya Rais Magufuli, kwahiyo Mdee hana hatia, Mahakama ina muachia huru na haki ya kukata rufaa ipo wazi”- amesema Hakimu Simba wa Mahakama ya Kisutu

Mdee alifikishwa mahakamani hapo kwa mara ya kwanza Julai 10, 2017.

Katika kesi ya msingi inadaiwa kuwa Julai 3, 2017 katika ofisi za makao makuu ya Chadema zilizopo mtaa wa Ufipa wilayani Kinondoni, Mdee alitamka maneno dhidi ya Rais John Magufuli kuwa, ‘anaongea hovyo, anatakiwa afungwe breki,’ kitendo kinachodaiwa kuwa ni kumdhalilisha Rais na kusababisha uvunjifu wa amani