Home | Terms & Conditions | Help

January 29, 2025, 2:50 am

NEWS: MAHAKAMA YAAMURU RAIS ZUMA ARUDISHWE GEREZANI

Mahakama ya Juu ya Rufaa ya Afrika Kusini imeamuru tena aliyekuwa Rais wa nchi hiyo Jacob Zuma kurejea gerezani baada ya kukubaliana na uamuzi wa awali kwamba ruhusa ya matibabu ilikuwa kinyume cha sheria.

Rais huyo mstaafu mwenye umri wa miaka 80 mwaka jana alihukumiwa kifungo cha miezi 15 kwa kudharau mahakama kutokana na kukataa kutoa ushahidi wake wakati wa uchunguzi wa ufisadi.

UPDATE: High court hears pleas to return to Zuma to prison - The Mail & Guardian

Kufungwa kwake kulisababisha maandamano ya ghasia katika jimbo la KwaZulu Natal na maeneo mengine ya Afrika Kusini na kusababisha vifo vya zaidi ya watu 300.

Zuma aliachiliwa baada ya miezi miwili jela, baada ya mawakili wake kubainisha kuwa alikuwa na ugonjwa usiojulikana.

Katika uamuzi wao wa siku ya Jumatatu, majaji walisema kwamba mamlaka ya magereza inapaswa kuamua ikiwa muda ambao rais huyo wa zamani ametumia kinyume cha sheria nje ya jela unapaswa kuhesabiwa kuelekea kifungo chake au la.

Mawakili wa rais huyo wa zamani walikuwa wamedai kuwa Zuma alihitaji matibabu ambayo hayangeweza kutolewa gerezani na sasa anaweza kupeleka suala hilo katika Mahakama ya Katiba.

Ni suala la kisheria lakini ambalo limekuwa na athari za kisiasa huko nyuma.

Kuna wasiwasi kwamba kurejea kwake gerezani kunaweza kusababisha kurudiwa kwa machafuko yaliyoonekana Julai.