- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MAHAKAMA YAAGIZA WEMASEPETU KUKAMATWA MARA MOJA
Dar es Salaam: Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imetoka hati ya kumkamata Miss Tanzania wa mwaka 2006, Wema Abraham Sepetu baada ya kukiuka masharti ya dhamana aliyopewa na mahakama hiyo.
Uamuzi huo umetolewa leo Jumanne Juni 11, 2019 na Hakimu Mkazi mwandamizi wa mahakama hiyo,Maira Kasonde baada ya mshtakiwa kushindwa kufika mahakama kusikiliza kesi inayomkabili kwa mara nyingine tena.
Novemba 1, mwaka jana Wema alipandishwa katika mahakama hiyo akikabiliwa na shtaka la kusambaza video ya ngono kupitia mtandao wa kijamii wa Instagram, kesi yenye jalada namba KJN/ RB/13607/2018-KUCHAPISHA NA KUSAMBAZA MAUDHUI YA NGONO MTANDAONI na aliachiwa kwa dhamana ya Sh. milioni 10 kupitia kwa Salim Limu.
Kabla ya kutoa uamuzi huo wakili wa Serikali, Silyia Mitanto amedia kesi hiyo ilikuja kwa ajili ya kusikiliza ushahidi lakini Wema na mdhamini wake wote hawakuwepo mahakamani. Baada ya kueleza hayo, Ruben Simwanza ambaye ni wakili wa Wema amesema mteja wake alikuwepo katika mahakama hiyo lakini aliugua tumbo na kulazimika kuondoka. Baada ya kusikiliza maelezo ya pande zote, hakimu Kasonde amesema,
“Kama amekuja mahakamani halafu akaondoka bila kutoa taarifa, mahakama itajuaje kama alikuja? Alishindwa nini kutoa taarifa mahakamani.” Baada ya kueleza hayo hakimu Kasonde ameahirisha kesi hiyo hadi Julai 4, 2019 huku akitoa hati hiyo ya Wema kukamatwa.
Shtaka linalomkabili Wema kwa mujibu wa sheria adhabu yake ni kulipa faini isiyopungua Sh20milioni ama kifungo kisichopungua miaka saba.