Home | Terms & Conditions | Help

November 23, 2024, 9:19 pm

NEWS: MAHAKAMA YA AFRICA KUTOA UWAMUZI KISI YA KINA MBOWE NA ZITTO

Mahakama ya Haki ya Afrika Mashariki leo Juni 17, 2020 inakusudiwa kutoa hukumu kwa njia ya mtandao ya maombi yaliyofunguliwa na baadhi ya viongozi wa vyama vya upinzani nchini Tanzania dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa serikali juu ya vifungu vya kisheria vinavyompa mamlaka Msajili wa vyama vya kisiasa nchini.

Waleta maombi (Applicants) hao waliwasilisha maombi yao katika mahakama hiyo mnamo Mei 27, Mwaka 2019 kuomba mahakama hiyo kutoa amri ya zuio la matumizi ya baadhi ya vifungu vya Sheria ya vyama vya siasa sababu vinaminya demokrasia nchini, utawala bora, pia vinakinzana na Mkataba wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Waleta maombi katika shauri Hilo ni Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe, Kiongozi wa ACT-WAZALENDO,Zitto Kabwe, M/Kiti wa CHAUMA Hashimu Rungwe, Makamu wa Zamani wa Rais wa Zanzibar na Katibu Mkuu wa CHADEMA Zanzibar, Kwa pamoja wanadai kuwa kutangazwa Kuanza kutumika kwa marekebisho ya mwaka 2019 ya Sheria ya vyama vya siasa, vyama vya siasa vipo Katika hatari ya kulazimishwa kutengeneza Sera za vyama zilizo kinyume na Itikadi zao pamoja na kupoteza wananchama.

Aidha Sheria hiyo inazuia watu kupata haki ya kutoa elimu ya uraia kwa vyama vya siasa hadi wapate kibali cha Msajili wa vyama vya siasa na pale watakapotoa elimu hiyo bila kibali wanaweza kukamatwa,kufungwa au kulipa faini suala ambalo litasababisha wananchi kukosa kupata elimu kuhusu uchaguzi.

Kwa pamoja waleta maombi wanadai kuwa Sheria hiyo inampa mamlaka Msajili wa vyama vya siasa nchini kuamua juu ya nani anapaswa kutoa elimu ya uraia na aina ya elimu itakayotolewa.

Tangu kuletwa kwa sheria hiyo mpya ya vyama vya siasa, kumekuwa na malalamiko mengi kutoka kwa wapinzani na hivi karibuni waliunda umoja wao unaoundwa na vyama kumi wakiazimia mambo mbalimbali pamoja na kutumia mikono ya sheria kuipinga.