- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MAGUFULI AKANUSHA TAARIFA ZA KIFO CHA WAZIRI MPANGO
Dar es Salaam. Rais wa Tanzania, John Pombe Magufuli amekanusha taarifa zilizosambaa mitandaoni zikieleza kuwa Waziri wa Fedha na Mipango Dkt Philip Mpango amefariki Dunia kitu ambacho sio kweli.
Rais amesema kuwa leo amefanya mawasiliano na Waziri huyo na kumueleza kuwa anaendelea vizuri na anamshukuru mungu.
Rais Magufuli amefafanua kuwa aliwasiliana naye kwa kutumiwa ujumbe mfupi wa maandishi na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango ambaye amelazwa Dodoma na kuomba kuusoma kwa kile alichokiita faida kwa waliokuwa wakidai waziri huyo amefariki dunia.
Ujumbe wenyewe huu hapa -“Mheshimiwa Rais, asante sana nimepata ujumbe wako kupitia kwa mke wangu, kwa neema ya Mungu naendelea vizuri, ninakula, ninafanya mazoezi ya kifua na kutembea, hao wanaonizushia kifo kwenye mitandao niliwaombea msamaha kwa Yesu wakati wa sala ya jioni jana.”
“Mheshimiwa Rais Mungu akubariki na akupe neema na ujasiri zaidi katika kuliongoza Taifa letu, katika wimbi hili naungana na wanafamilia katika kuomboleza kifo cha Katibu mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi, Rest in Peace,” amesema Magufuli akimnukuu Dk Mpango.
Akifafanua kuhusu ujumbe huo Magufuli amesema, “ni huyo ambaye aliambiwa jana amekufa, yeye amesema katika sala yake jana jioni aliwaombea msamaha kwa Yesu.”
Mkuu huyo wa nchi ametoa kauli hiyo hii leo Ijumaa Februari 19, 2021 katika ibada ya mazishi ya aliyekuwa katibu mkuu kiongozi, Balozi John Kijazi katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.
Amesema ulipoingia ugonjwa wa kubana na mafua mwaka 2020 Tanzania iliushinda kwa sababu ya kumtanguliza Mungu na juhudi mbalimbali.
Hiyo ni kutokana na kile kinachoaminiwa kuwa kama kitu huwezi kukitatua mtangulize Mungu kwa sababu ndiye mweza wa yote.
“Magonjwa yapo na yatendelea kuwepo, magonjwa ya kupumua na vifua pia yataendelea kuwepo na hayakuanzia hapa kwani zipo nchi zilizopoteza watu wengi lakini Tanzania Mungu ameisaidia katika mwaka uliopita."