Home | Terms & Conditions | Help

April 4, 2025, 7:42 am

NEWS: MAFUNZO YA JKT YASITISHWA KWA MUDA, WALIOKO KAMBINI WARUDISHWA MAJUMBANI

Dodoma. Jeshi la Kujenga Taifa nchini (JKT) limesitisha kwa muda mafunzo ya kujitolea kwa kambi zote nchi nzima, kwa mwaka 2020/21 yaliyokuwa yanatarajiwa kuanza hivi karibuni.

Akizungumza leo Januari 19, 2021 katika ofisi ya JKT Chamwino Dodoma kaimu mkuu wa utawala wa jeshi hilo, Kanali Hassan Mabena amesema mafunzo hayo yamesitishwa kutokana na sababu za ndani ya jeshi hilo.

Kanali Mabena amesema kutokana na kusitishwa kwa mafunzo hayo, JKT inawataka vijana wote waliochaguliwa kuripoti kwenye kambi kwa ajili ya kuhudhuria mafunzo hayo kurudi majumbani mwao.