- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MAELFU YA WAOMBOLEZAJI WAJITOKEZA KUMUAGA GEORGE FLOYD
Maelfu ya watu walijitokeza kutoa heshima zao za mwisho mjini Houston jimbo la Texas katika hafla ya Kumuaga Mmarekani mweusi aliyeuwawa kikatili na Polisi nchini Marekani.
Jeneza lake lililokuwa wazi lilipelekwa katika kanisa la The Fountain of Praise ambapo karibu watu 6,000 walifika kumuaga. Mgombea wa urais wa chama cha Democratic Joe Biden, alikutana na wanafamilia ya Floyd.
Floyd Atazikwa leo kando ya kaburi la mamake katika hafla ya faragha.
George Floyd, Mmarekani mweusi mwenye umri wa miaka 46 ambaye mauaji yake na polisi mweupe yamembadilisha kuwa picha ya ulimwengu ya mapambano dhidi ya ubaguzi wa rangi na ukatili wa polisi, atazikwa leo mjini Houston, ambako alikulia.
Waombolezaji wengi walitengeneza ishara ya msalaba wakati wakikaribia jeneza la Floyd lililokuwa wazi, katika kanisa la The Fountain of Praise mjini Houston, jimbo la Texas, kutoa heshima zao za mwisho wakati wengine wakipiga magoti au kuinamisha vichwa na kumuombea kimyakimya mtu ambaye amekuwa ishara ya karibuni ya vuguvugu la kupinga ubaguzi wa rangi Marekani.
Hafla hiyo ilikuwa ya mwisho katika msururu wa hafla zilizoandaliwa za kumuaga Floyd. Atazikwa leo katika mazishi ya faragha kando ya kaburi la mamake mjini Houston, ambako ndiko alikokulia.
Mjini Washington, wajumbe wa Democratic walipiga magoti na kusalia kimya kwa dakika nane na sekunde 46, muda alioutumia polisi mweupe kugandamiza shingo ya Floyd akitumia goti.