- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MADIWANI TABORA WAKOSOA UTEUZI WA RAIS SAMIA
Tabora. Baraza la Madiwani wa Manispaa ya Tabora wamesikitishwa vikali na uamuzi wa Rais Samia Suluhu Hassan alioufanya wa kumteua aliyekuwa Mkuu wa Wilaya wa Tabora Dk Yahaya Nawanda kuwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu.
Dk Nawanda alikuwa Tabora na sasa anakwenda kuchukua nafasi ya David Kafulila ambaye kwenye mabadiliko hayo amewekwa kando.
Dk Nawanda ni miongoni mwa wakuu wa wilaya waliopandishwa kuwa wakuu wa mikoa katika mabadiliko aliyoyafanya Rais Samia usiku wa kuamkia leo Alhamisi Julai 28, 2022.
Akizungumza katika Baraza la Madiwani leo hii Alhamisi Julai 28, 2022, Meya wa Manispaa ya Tabora, Ramadhan Kapela amesema wamesikitishwa kuondoka kwa Dk Nawanda ingawa wanafurahi kupandishwa kwake kuwa mkuu wa mkoa.
"Tunasikitishwa kuondoka kwake (Dk Nawanda) kwani alikuwa anashirikiana nasi vizuri lakini tunafurahi anaenda kuwa mkuu wa mkoa," amesema
Amesema baada ya kuondoka kwake, wanatamani Rais Samia ateue mkuu wa wilaya mwenye sifa kama za Dk Nawanda ambaye hakuwa na makuu.
Dk Nawanda aliteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Tabora mwaka Juni 2022.