- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MABOSI WA MAMLAKA YA BANDARI WAFIKISHWA MAHAKAMANI
Dar es Salaam. Waliokuwa wafanyakazi wa ngazi za juu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) wamefikishwa leo Juni 30,2022 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashtaka matatu, likiwamo la kuisababishia mamlaka hiyo hasara ya Dola za Marekani 1.85 milioni sawa na Sh4.2 bilioni za kitanzania.
Washtakiwa hao ni aliyekuwa Ofisa Rasilimali watu, Peter Gawile (58), aliyekuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Manununuzi, Casmily Lujegi (65).
Wengine ni aliyekuwa Mkurugenzi wa Idara ya Manununuzi, Mashaka Kisanta (59) na Kilian Chale (51) ambaye alikuwa Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano.
Wamefikishwa mahakamani hapo leo, Juni 30, 2022 na kusomewa mashtaka na wakili wa Serikali, Timotheo Mmari akisaidiana na Mosia Kaima, mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Ramadhani Rugemalira.