- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MABOSI TPA WAFIKISHWA MAHAKAMANI
Wafanyakazi saba(7) wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) na Wakili wa Kujitegemea kutoka Kampuni ya Mnengele &Associates na ELA Advocatee leo Juni 12, 2020 wamepandishwa katika Mahakama ya Haki mkazi Mwanza na kusomewa mashitaka 94 yakiwemo kuongoza genge la uhalifu, wizi, kughushi, kutoa nyaraka za uongo, kutakatisha fedha pamoja na kusababishia TPA hasara zaidi ya Tsh 8.3 Billion.
Watuhumiwa hao wanashtakiwa kwa tuhuma za rushwa , uhujumu uchumi pamoja na wizi wa wa fedha zaidi ya Sh.bilioni nane mali ya Mamlaka ya Bandari Tanzania(TPA. Watuhumiwa hao waliokuwa wanachunguzwa na TAKUKURU makao makuu ni aliyekuwa Mhasibu Mwandamizi TPA Makao Makuu Deogratius Lema na aliyekuwa Mhasibu Mwandamizi TPA Makao MakuuAike Mapuli aliyekuwa Mhasibu Mwandamizi TPA Makao.
Washtakiwa hao ni aliyekuwa Ofisa Uhasibu TPA Makao Makuu Marystella Minja, aliyekuwa Mhasibu wa Kituo cha Bandari ya Mwanza Thomas Akile, aliyekuwa Mhasibu Msaidizi wa Kituo cha Bandari Mwanza Ibrahim Lusato na aliyekuwa Keshia wa kituo cha bandari Mwanza Wendelin Tibuhwa, aliyekuwa Ofisa Kodi wa Kituo cha Bandari Mwanza James Mbedule pamoja na Wakili wa kujitegemea kutoka Kampuni ya Mnengele &Associates na ELA Advocatee Leocard Kipengele .
Washitakiwa wote wamepelekwa Gerezani kwa kuwa mashitaka ya kutakatisha fedha hayana dhamana. Kesi imeahirishwa na itatajwa tena Juni 26 mwaka huu.