Home | Terms & Conditions | Help

January 22, 2025, 2:08 pm

News: Maamuzi ya Jeshi la polisi kuwafukuza askari polisi wake wa tatu.

MWANZA: Jeshi la Polisi Mkoani Mwanza la watimua watumishi wake watatu kwa kosa la kukiuka maadili ya jeshi hilo kwa kujihusisha na viendo vya uhalifu.


Akiongea na Muakilishi wetu Kamanda wa Polisi mkoa wa MWANZA, AHMED MSANGI "amesema kuwa uamuzi huo umechukuliwa na jeshi hilo ili iwe fundisho kwa askari wengine ambao hawazingatii weledi wakati wa utekelezaji wa majukumu yao"


Akizungumza na Watendaji wa Jeshi la polisi mkoani MWANZA wakati wa kikao cha kazi kilichofanyika kufuatia ongezeko la matukio ya ukiukwaji wa maadili miongoni mwa baadhi ya Watendaji hao, Kamanda MSANGI amesema vitendo hivyo havivumiliki.

Kamanda MSANGI ametumia kikao hicho kuwakumbusha Watendaji wa Jeshi la Polisi mkoani MWANZA kuzingatia weledi wakati wa kutekeleza majukumu yao na kufanya kazi zao bila kumuogopa wala kumuonea mtu yoyote.