Home | Terms & Conditions | Help

November 23, 2024, 7:32 pm

NEWS: MAALIM SEIF KUPIGANIA TENA NAFASI YA URAIS, ACHUKUA FOMU.

Maalim Seif Sharif Hamad Mwanasiasa mkongwe nchini Tanzania aliyekipigania kiti cha urais kwa zaidi ya miongo 2 jana Jumapili, alichukua fomu za kugombea urais wa Zanzibar mwezi Oktoba mwaka huu. Hii itakuwa mara ya sita kwa Maalim kugombea, akishindwa katika mara tano zilizopita.

Maalim ameshiriki Uchaguzi Zanzibar tangu uchaguzi wa kwanza chini ya mfumo wa vyama vingi uliofanyika Tanzania nzima mwaka 1995. Mwanasiasa huyo mwenye umri wa miaka 76 kwa sasa, alikiongoza chama cha CUF kwa upande wa Zanzibar katika mbio za Urais.

Baada ya kushindwa kukitwaa kiti hicho, miaka mitano baadaye 2000 alijaribu tena na hakufanikiwa vile vile. Matokeo ya uchaguzi huu yalisababisha ghasia za kisiasa Januari 2001.

Mkasa wa mauaji ya 2001 ulihusisha wanachama wa CUF walioamua kuandamana kwa amani kupinga matokeo ya uchaguzi, wakiamini chama chao kimeporwa ushindi, kwa upande mwengine vikosi vya usalama vikiongozwa na Jeshi la Polisi viliyazima maandamano hayo kwa risasi za moto.

Kwa mujibu wa ripoti ya Human Rights Watch (HRW) iliyopewa jina, "Tanzania: Risasi zilinyesha kama mvua", inakisia watu 35 waliuwawa, wapatao mia sita walijeruhiwa na takribani 2000 walikimbilia nchi jirani.