- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MAALIM SEIF AMKABA KOO MEMBE AMTAKA AKAE PEMBENI
Dar es Salaam. Mwenyekiti wa chama cha ACT- Wazalendo, na Mgombea Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya ACT Wazalendo Maalim Seif Sharif Hamad ameonesha masikitiko yake juu ya kauli ya mgombea urais kupitia chama chake hicho Bernard Membe kutaka kufanya kampeni wakati chama hicho kimetangaza kumuunga mkono mgombea wa Chadema, Tundu Lissu.
Maalim Seif ameeleza hayo leo Jumanne Oktoba 20, 2020 katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam .
Membe jana katika mkutano wake na wanahabari aliahidi kuendelea na kampeni siku nane zilizobaki kabla ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 28, 2020 na akiahidi kushinda uchaguzi huo.
Membe alifanya mikutano mitatu ya kampeni kati ya Agosti 26 na Septemba 3, 2020 kwenye mikoa ya Pwani na Mtwara na tangu kipindi hicho hajawahi kuonekana jukwaani hadi alipoibuka jana na kueleza kwamba atafanya kampeni za lala salama.
"Chama chetu cha ACT Wazalendo katika mkutano mkuu tuliamua kuwa tunataka mabadiliko kama hatutashirikiana hatutaweza kuiondoa CCM,” amesema Maalim Seif akibainisha kuwa msimamo huo walimwambia Membe ambaye jana katika mkutano wake na wanahabari alieleza kutokuwa na imani kuwa wapinzani wanaweza kuungana na kuing’oa CCM madarakani, bali mpasuko ndani ya chama tawala ndio unaweza kuwapa wapinzani ushindi.
“Alipokuja (Membe- kutoka CCM kujiunga ACT) tulimwambia kabisa maamuzi ya mkutano mkuu tushirikiane na vyama vingine akakubali. Sasa Membe anasema anaendelea na kampeni, mmeona kampeni?"
"Tulikaa wiki moja na nusu kuona kampeni zikisuasua, tukaitana kamati ya uongozi na Membe alikuwepo. Tukasema mgombea wetu haonekani yaani hata mzee wa ubwabwa anaonekana,” amesema Maalim.
Amesema katika kikao hicho Membe alitoa muda maalum akisema ikishindikana waunge mkono mgombea mwingine.
"Sasa amesema ataanza kampeni, haya tuone kampeni zake. Nia yake ni kuwachanganya Watanzania. Mgombea anayeelekea kushinda ni Lissu na jana nilikuwa naye Moshi kwenye mkutano mkubwa," amesema Maalim Seif.
Maalim Seif amesema kauli yake ya kumuunga mkono Lissu ambayo inafanana na iliyotolewa na kiongozi wa chama hicho, Zitto Kabwe si kauli zao binafsi kama alivyodai Membe, bali ni msimamo wa chama hicho.
"Zitto alitoa kauli ya chama si kauli yake. Kiongozi wa chama ndiyo msemaji mkuu wa chama. Mimi kama mwenyekiti wa chama na moja kati ya kazi yangu ni kusimamia maamuzi ya chama,” amesema.
Alipoulizwa kama kuna mgogoro ndani ya chama hicho, Maalim Seif amesema, “hakuna mgogoro ila Membe anataka kuonyesha hivyo."