Home | Terms & Conditions | Help

November 23, 2024, 5:05 pm

NEWS: LISSU AZUILIWA NA POLISI KWENDA KIBAHA

Msafara wa Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo ( CHADEMA ) na Mgombea Urais kupitia chama hicho Tundu Lissu umezuiwa kuendelea na safari katika eneo la Kiluvya Gogoni mpakani mwa Dar es salaam na Pwani kuanzia majira ya saa tano asubuhi hii leo mpaka Jioni hii.

Lissu na Msafara wake walikuwa wakielekea Kibaha Mkoani Pwani kufanya kikao cha ndani cha wanachama wa Chadema na Kutembelea Soko la Kibaha.

Msafara huo umezuliwa na magari manne ya Jeshi la Polisi mkoa wa Pwani yaliyosheheni askari wenye sare na silaha za moto na mabomu ya machozi.

Lissu amesema kuwa anajua kuwa Polisi hao wametumwa na viongozi wao huko juu kwahiyo atabaki katika eno hilo mpaka pale atakaporuhusiwa kwenda kibaha.

Kwa upande wake, kamanda wa Polisi mkoa wa Pwani Wankyo Nyigesa amesema kitendo cha Tundu Lissu kwenda kufungua matawi ya CHADEMA ni shughuli ya kichama na kisheria Jeshi la polisi linapaswa kipewa taarifa saa 48 kabla ya tukio husika .