- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: LISSU AAHIDI KUIVUNJA TUME YA UCHAGUZI
Mgombea wa Urais kwa tiketi ya Chadema Tundu Lissu ameahidi kuwa iwapo atachaguliwa katika uchaguzi mkuu ujao, ataivunja Tume ya Taifa ya Uchaguzi pamoja na kuitisha upya uchaguzi wa serikali za mitaa.
Mgombea urais huyo kwa tiketi ya CHADEMA ameyasema hayo jana Septemba 25, 2020 katika mkutano wake wa kampeni mjini Misungwi, baada ya msimamizi wa uchaguzi katika jimbo hilo kuwaengua wagombea udiwani wote wa kata 27 za jimbo hilo pamoja na mgombea ubunge wa chama hicho Shija shimbi .
Lissu ameendelea na kampeni katika majimbo ya Misungwi, Kwimba, Sumve, Magu na Nyamagana mkoani Mwanza
Akiwa Hungumalwa wilayani Kwimba, mgombea urais huyo wa Jamhuri ya Muungano Mh. Tundu Lissu amesema akichaguliwa kuongoza nchi atakomesha mfumo wa Stakabadhi Ghalani aliodai unawakandamiza wakulima .
Akihutubia wakazi wa jiji la Mwanza katika uwanja wa Kleruu Mabatini, Mgombea Urais huyo, ametangaza neema kwa watumishi wa vyombo vya dola, wakiwemo wanajeshi, askari polisi na kada zingine za elimu na afya, ambao amedai kwa miaka mitano iliyopita hawajawahi kupewa nyongeza ya mishahara.