- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: LIPUMBA AMSHAURI SAMIA KURUDISHA KATIBA MPYA
Mwenyekiti wa chama cha wananchi CUF, Prof. Ibrahim Lipumba, amemuomba Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassani kutumie uzoefu wake kama Makamu Mwenyekiti wa Bunge la Katiba kukamilisha mchakato wa kupata Katiba mpya itokanayo na maoni ya wananchi waliowengi.
Prof. Lipumba aliyasema hayo mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam, wakati akizungumza na waandishi wa habari na kueleza kuwa inabidi kuwapo na utashi wa kisiasa kutoka uongozi wa juu kuwa sekta binafsi ni muhimili muhimu wa kukuza uchumi wa nchi.
Aidha, Prof. Lipumba alitaka uwekwe utaratibu wa kuwatumia wataalamu wa afya kuzifanyia uchunguzi chanjo za corona na majibu ndiyo yaongoze kuamua kuhusu kutumia au kutotumia chanjo hizo.
Alisema kwa sababu usafiri wa ndege kimataifa una ushindani mkubwa, serikali ijiimarishe safari za ndani
Pia alimuomba Rais Samia kuangalia uwezekano wa kutafuta msaada au mkopo usiokuwa na riba ili kuweza kuwezesha kukamilika kwa mradi wa ujenzi wa reli ya Standard Gauge pamoja na ule wa kufua umeme mto Rufiji.
Prof. Lipumba alisema Rais Samia yupo katika kipindi cha kupendwa na kueleweka na kumuomba akitumie vizuri ndani na nje ya nchi ili awe rais wa kwanza wa Tanzania kushinda tuzo ya Mohamed Ibrahimu.