- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: LAZARO NYALANDU AREJEA CCM, KWA KISHINDO
Dodoma. Aliyewahi kuwa Waziri wa Maliasili na Utalii nchini na Aliyekuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Lazaro Nyalandu ametangaza kurejea katika Chama Cha Mapinduzi (CCM) akitokea chama kikuu cha Upinzani nchini Chadema na kusema kazi iendelee.
Nyalandu ametangaza uamuzi huo leo Aprili 30, 2021 mbele ya Mkutano Mkuu Maalum wa CCM ilifanyika jijini Dodoma.
Mbunge huyo wa zamani wa Singida Kaskazini akisalimia wajumbe wa Mkutano huo mara baada ya kukaribishwa na Mwenyekiti wa Chama hicho, Samia Suluhu Hassan, Nyalandu amesema ameamua kurejea nyumbani huku akisisitiza kuwa kazi iendelee.
“Kupitia Mkutano huu Maalum wa CCM naomba kukushukuru Mwenyekiti (Rais Samia) kwa kukubali Kunipokea, kunisamehe na kuniruhusu kurejea nyumbani (CCM), hakuna furaha inayozidi furaha ya Mtoto arejeapo nyumbani” amesema Lazaro Nyalandu baada ya kurejea CCM
“Katika Nchi ya ugenini wimbo hauimbiki, Mzee Lowasa, Mzee Sumaye, Mzee Slaa hawa ni Mashuhuda wachache kati ya wengi wa kwanini wimbo wa Bwana hauimbiki katika Nchi ya ugenini”
“Watanzania wameiona nyota yako Rais Samia, wameguswa kwa kuinuliwa kwako kwakuwa Mungu alikuandaa kuwa Kiongozi wa Taifa hili, Mungu akuongoze katika safari, uwepo wangu kwenye Mkutano huu ni kielelezo tosha cha wewe kuungwa mkono na Watanzania wote”
“Kazi iendelee, Rais wetu (Samia Suluhu), Mama yetu, Mwenyekiti wa Chama chetu (CCM), Mama tuma neno lako likaponye wote walioumia, ukaitwe heri na shujaa wa mioyo ya Watanzania, ukaongeze Tabasamu katika nyuso za Watanzania wote”NYALANDU
Nyalandu alitangaza kujiondoa CCM mwaka 2017 akisema amechukua uamuzi huo kutokana na kutokuridhishwa na mwenendo wa siasa nchini Tanzania, ukiukwaji wa haki za kibinadamu, ongezeko la vitendo vya kidhalimu dhidi ya Raia na kutokuwepo kwa mipaka baina ya mihimili ya dola, Serikali, Bunge na Mahakama.