Home | Terms & Conditions | Help

January 29, 2025, 2:33 am

NEWS: KOCHA WA SIMBA AKUTWA NA MADAWA YA KULEVYA

Dar es Salaam. Kocha wa Club ya Simba Muharami Sultan (40) amekamatwa na Dawa za kulevya aina ya Heroine na Bangi na Mammlaka ya Kupambana na Dawa za Kulevya nchini (DCEA).

kocha huyo amekamatwa yeye na watuhumiwa wengine 11 akiwemo mmiliki wa kituo cha Cambiasso Sport Academy kilichopo Tuangoma, Kambi Zuberi seif, Said Matwiko mkazi Magole.

Hayo yameelezwa leo Novemba 15 na Kamishna Jenerali wa DCEA, Gerald Kusaya alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.

Muharami Sultani na wenzake hao wanadaiwa kukutwa na kilo 34.89 za dawa za kulevya aina ya heroin na biskuti 50 zilizotengenezwa kwa kutumia dawa ya kulevya aina ya bangi.