- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: KIONGOZI WA UPINZANI VENEZUELA ALIOMBA JESHI KUSUSIA UCHAGUZI
Kiongozi kinara wa upinzani nchini Venezuela Juan Guaido amelitaka jeshi la nchi hiyo kususia uchaguzi wa bunge unaopangwa kufanyika Desemba mwaka huu na kusaidia kuongeza shinikizo la kimataifa dhidi ya Rais Nicolas Maduro.
Guaido akihutubia hii leo kupitia mitandao ya kijamii ameuomba uongozi wa kijeshi kujiunga katika kile alichokiita "muafaka wa umoja” wa nguvu za upinzani kuzuia kuandaliwa kwa uchaguzi wa Desemba 6. Guaido amewaambia wanajeshi kuwacha kujificha katika sketi za kiongozi ambaye ni dikteta na kukoma kupuuza ukweli wa mambo nchini Venezuela. Jeshi linaonekana kuwa nguzo muhimu ya utawala wa Maduro, pamoja na washirika wake Urusi na Iran.
Guaido na viongozi wakuu wa upinzani wameapa kususia uchaguzi wa Desemba 6 kuhusiana na ukosefu wa uwazi baada ya Mahakama ya Juu inayomuunga mkono Maduro kuwateuwa maafisa wa uchaguzi – jukumu ambalo lingestahili kufanywa na bunge ambalo linadhibitiwa na wajumbe wengi wa upinzani.
Karibu vyama 37 vya upinzani vinaunga mkono kususia uchaguzi na kile kinachofahamika kama muafaka wa "kuongeza shinikizo la kimataifa dhidi ya udikteta,” kwa mujibu wa Guaido.